Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete asisitiza mambo muhimu kwa wananchi

PWANI-Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewahimiza wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.
Wito huo ameutoa baada ya kushiriki katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Ally Hapi katika Wilaya ya Bagamoyo.
Katika ziara hiyo walitumia nafasi kueleza mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mwaka 2020 hadi 2025.
Pia, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete aliwahimiza wananchi kuendelea kuamini kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan bado inaendelea kutekeleza majukumu yake na yanakwenda vizuri.

"Hivyo tuna kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan."

#KaziInaendelea

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news