Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete azindua Zahanati ya Kijiji cha Tonga, akabidhi vifaa tiba

PWANI-Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete tarehe 11 Septemba, 2024 amefungua zahanati katika Kijiji cha Tonga.
Amesema, hiyo ni moja kati ya zahanati 11 zilizokamilishwa katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020-2025.
Vilevile, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amekabidhi vifaa tiba kwa ajili ya kuhudumia wananchi na baadae alizungumza na wananchi wa kijiji hicho.
Katika kikao hicho, Mheshimwa Ridhiwani Kikwete amewahimiza wananchi kujitokeza wakati wa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na baadae kupiga kura.
Pia katika mkutano huo,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete aliendelea kumshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maendeleo makubwa waliyoyafikia na misaada mbalimbali anayowafikishia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news