Lengo ni kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma-Katibu Mkuu Abeida

ZANZIBAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar,Bi.Abeida Rashid Abdallah amesema, miongozo na sera inayohusu watu wenye ulemavu kwa sasa haitoshelezi hivyo ipo haja ya kuangalia sera na sheria zingine namna ilivyowajumuisha watu hao ili kuhakikisha kwamba hakuna kundi ambalo limeachwa nyuma katika jamii.
Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akifungua mkutano wa programu ya Kimataifa ya Haki za Watu Wenye Ulemavu, uliyofanyika katika ukumbi wa Goden Tulip, Uwanja wa Ndege, Unguja.

Amesema, Sera ya mwaka 2004 inayohusu watu wenye ulemavu haitoshelezi, hivyo ipo haja ya kuangalia sera na sheria zingine namna ilivyowajumuisha watu wenye ulemavu.
Alieleza kuwa,kama hakuna basi watu wenye ulemavu wanalazimika kupaza sauti zao kwa kuwaambia jamii changamoto zinazowakabili kutokana na mapungufu yaliyopo kwenya sera na sheria iliyopo.

"Miongozo na Sera ya 2004 ambayo inawajumuisha watu wenye ulemavu ipo ambapo kupitia programu hii ya kikao cha leo inafanyiwa review hivyo lazima tushukuru. Lakini pale ambapo tunaona mapungufu lazima tuwaoneshe wenzetu nini tunahitaji,” amesema Abeida.
Aidha,Abeida amesema muda sio mrefu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itazindua Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kumpambana na vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ambapo Mpango huo umezingatia masuala ya watu wenye ulemavu.
Pia alitoa wito kwa watu wenye ulemavu kuweka takwimu zao ingawa Serikali inaweka, lakini ni vyema na wao wenyewe kuweka takwimu zao vizuri ili ziweze kuwasaidia wakati wa kutoa maoni yao.

Mwisho, Bi.Abeida amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suhuhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa uongozi wao pamoja na kuzingatia masuala ya usawa wa kijinsia na masuala ya watu wenye ulemavu.
Mapema akizungumza Mtaalamu wa Ushauri masuala ya Usawa wa Kijinsia,Bi.Maja Hansen amesema,mkutano huo wa Haki za Watu Wenye Ulemavu umelenga kuzungmzia ajenda nne ikiwemo Ushiriki na Ushirikishaji, Ulinzi wa vitendo vya ukatili kwa Watu Wenye Ulemavu, Maboresho ya Sera, na Masuala ya takwimu ambapo anaamini mkutao huo utaleta tija.
Kwa upande wa washiriki wa mkutano huo,Ali Omar Makame kutoka Shirikisho la Jumuiya la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) amesema, amefurahishwa na hatua ya waandaji wa mkutano huo walivyowashirikisha watu wenye ulemavu katika kikao hicho, kwani wataweza kueleza changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa vyoo rafiki kwa baadhi ya majengo ya Serikali na binafsi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news