Mkalama yatangaza mkakati wa kupambana na Homa ya Nyani

SINGIDA-Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe.Moses Machali amewataka Wakuu wa Idara, Watumishi wa Afya, Watendaji Kata na Vijiji pamoja na Maafisa Tarafa wilayani Mkalama kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujilinda na ugonjwa wa Homa ya Nyani maarufu kama Mpox.
Wito huo ameutoa leo Septemba 5,2024 wakati wa kikao cha afya ya msingi wilayani Mkalama kilichofanyika kwenye ukumbi ulipo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.

"Wakuu wa Idara, watumishi wa afya, Watendaji kata na Vijiji pamoja na Maafisa Tarafa kwa pamoja twendeni tukaelimishe jamii kuhusu homa ya nyani na namna ya kujilinda na ugonjwa huu."

Aidha,katika kuhakikisha wananchi wanajilinda na ugonjwa huo, Mhe. Moses Machali amepiga marufuku wananchi kusalimiana kwa kupeana mikono ili kujilinda na ugonjwa huo.
"Kuanzia leo tusisalimiane kwa kupeana mikono, tukifanya hivi tutajilinda na sisi na kuwalinda wengine,"amesema Mhe. Machali.

Vile vile Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali ametoa agizo kuwekwa maji yanayotiririka pamoja na sabuni katika maeneo yote ya taasisi za umma pamoja na yale yenye watu wengi.

Awali akiwasilisha hali ya ugonjwa huo, Afisa Afya Wilaya ya Mkalama,Dorice Damiani amesema kuwa ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kushikana mikono, kujamiana na mtu mwenye ugonjwa huo pamoja na kuchangiana nguo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news