Mkoa wa Mwanza utanufaika na fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali-Waziri Dkt.Nchemba

MWANZA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mohamed Mtanda na wakazi wote wa mkoa huo, kwamba Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itahakikisha kuwa miradi yote ya kimkakati na mingine yote inayogusa maisha ya wananchi mkoani humo itaendelea kupatiwa fedha ili kusisimua uchumi wa nchi pamoja na kuboresha maisha ya wananchi wa mkoa huo.
Mhe. Dkt. Nchemba aliyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mkoa huo pamoja na Kamati ya Usalama ya Mkoa, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 7 ya kukagua, kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua baadhi ya miradi aliyopangiwa katika mkoa wa Mwanza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mohamed Mtanda, alimpongeza Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha nyingi zinazotumika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati ya Daraja la Kigongo-Busisi (Daraja la JPM), upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, miradi ya sekta za elimu, maji, miundombinu na mingine mingi yenye manufaa makubwa kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news