Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ateta na wadau mbalimbali kando ya Mkutano wa GlobE Network jijini Beijing

BEIJING-Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU),Bw. Crispin Francis Chalamila, amemtembelea Balozi wa Tanzania nchini China,Mhe. Khamis Mussa Omar kwa lengo la kujitambulisha.
Mkurugenzi Mkuu akikabidhi souvenir kwa Mhe. Balozi wa Tanzania nchini China.

Akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu, Balozi Omar jijini Beijing ameipongeza TAKUKURU kwa jitihada inazozifanya katika kuzuia na kupambana na rushwa.

Pia,ameisisitiza TAKUKURU kutumia vema fursa ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na ya China,kwani kuna mambo mengi ya kujifunza.
Mkurugenzi Mkuu alikuwa Beijing China kuhudhuria The 5th GlobE Network Meeting uliofanyika Septemba 24 hadi 27, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine amelisilisha mada kuhusu Mfumo wa Sheria wa Tanzania kwenye Mapambano dhidi ya Rushwa.
Mkurugenzi Mkuu akizungumza na Bw. Cheng Long - Senior Inspector Department of International Cooperation - China National Commission of Supervision.

Vilevile, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila alitumia mkutano huu kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa baadhi ya Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa walioshiriki Mkutano wa GlobE Network jijini Beijing China kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya TAKUKURU na mamlaka hizo.

Viongozi aliokutana nao ni kutoka National Commission of Supervision ya China Beijing (NCS), Independent Commission Against Corruption (ICAC) ya China Hong Kong na National Prosecutions Authority - (NPA) ya Afrika Kusini.
Mkurugenzi Mkuu akizungumza na Bibi. Shamila Batohi - National Director of Public Prosecution ya Afrika Kusini.
Mkurugenzi Mkuu baada ya mazungumzo na Bw. Bryan Chong, Director of Corruption Prevention - Independent Commission Against Corruption ya Hongkong China.

Mazungumzo ya Mkurugenzi Mkuu na viongozi hao yalilenga maeneo yafuatayo:

📌 MAFUNZO YA UCHUNGUZI

📌 UFUATILIAJI NA UREJESHWAJI WA MALI

📌 FORENSIC EVIDENCE

📌 INTELIJENSIA

📌 UZUIAJI RUSHWA

📌 UELIMISHAJI UMMA

📌 VITENDEA KAZI pamoja na

📌 ZIARA ZA MAFUNZO

Kwa ujumla wake viongozi hao wamepongeza jitihada za TAKUKURU katika Kuzuia na Kupambana na Rushwa pamoja na ushirikiano walionao Kikanda na Kimataifa na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news