Mkusanya ushuru Siha kizimbani kwa makosa mawili

NA DIRAMAKINI

JUMANNE Ramadhani Mhando ambaye ni mkusanya ushuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Mhando amefunguliwa shauri shauri la jinai Na 27222/2024 leo Septemba 24, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, mbele ya Mheshimiwa Herrieth Mhenga

Mshtakiwa anakabiliwa na makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni kosa la rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (sura ya 329).

Aidha, kosa la pili ni kukaidi kutekeleza jukumu la kisheria kinyume na kifungu cha 123 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura 16 marejeo ya mwaka 2019.

Mshtakiwa alijipatia kiasi cha shilingi 2,925,350 ikiwa ni manufaa yaliyotokana na ushuru aliokusanya kwa kutumia Mashine ya POS.
Aidha, mshtakiwa amekana makosa yote na yupo nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya damana.Shauri hilo litakuja kwa masikilizo ya awali Oktoba 15,2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news