Mkutano wa 47 wa SADC-CISNA kuanza kesho hadi Oktoba 4 jijini Zanzibar

NA GODFREY NNKO

MKUTANO wa 47 wa Mwaka wa Kamati ya Mamlaka za Usimamizi wa Bima,Masoko ya Fedha na Taasisi za Fedha zisizo za Kibenki (CISNA) chini ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kuanza kesho Septemba 29 hadi Oktoba 4,2024 jijini Zanzibar.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 28,2024 na Sekretarieti ya Maandalizi ya Mkutano huo ambapo utafanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Airport jijini humo.

Ikumbukwe kuwa,SADC Committee of Insurance, Securities and Non-banking Financial Authorities (CISNA), mkutano wa 46 ulifanyika huko Swakopmund nchini Namibia mwaka jana.

Aidha, mwaka huu wenyeji wa mkutano huu wa 47 hapa nchini ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

CISNA ni kamati ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), iliyoanzishwa mwaka 1998, kufuatia Kifungu cha 10 cha Itifaki ya SADC kuhusu Fedha na Uwekezaji.

Ni kamati ya mamlaka inayosimamia bima, usalama, na taasisi za kifedha zisizo za kibenki katika nchi wanachama wa SADC.

Aidha,CISNA ni sehemu ya Idara ya Fedha, Uwekezaji na Forodha ya Sekretarieti ya SADC na inaripoti kwa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa SADC.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkutano huo ambao unajumuisha mikutano mbalimbali itawaleta pamoja washiriki kutoka mamlaka 26 za wanachama kutoka nchi 14 za SADC.

Sambamba na wanachama wa Baraza la Utawala, Kamati Ndogo, Vikundi Kazi vya Kiufundi na wawakilishi kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, Mifumo ya Kimataifa, Mashirika ya Kanda na mamlaka za wanachama.

Aidha, zaidi ya washiriki 110 wamesajiliwa kwa ajili ya kuhudhuria ana kwa ana, na mikutano itafanyika kwa mfumo wa mchanganyiko ili kuwezesha ushiriki wenye matokeo makubwa.

Vile vile, taarifa hiyo imefafanua kuwa, Septemba 29 hadi 30, 2024 Kamati Ndogo ya Masoko ya Mitaji (CMS), Bima na Mfuko wa Pensheni, Mifumo ya Matibabu na Wakala (IRMIS), na Kamati Ndogo ya Huduma Ndogo za Fedha na Ushirikiano wa Kifedha (MiFFCO) zitaandaa mikutano ili kupitia maendeleo ya malengo ya kimkakati yaliyoainishwa katika Mpango wa Kimkakati wa CISNA 2022 hadi 2026.

Pia, Septemba 30, 2024 kamati hizo tatu zitakutana kwa pamoja kujadili masuala ya sekta mbalimbali na kupokea taarifa kutoka kwa Vikundi Kazi vya Kiufundi kuhusu maeneo muhimu kama vile AML/CFT/CPF.

Pamoja na Elimu na Ulinzi wa Kifedha kwa Watumiaji, maendeleo ya Fintech, na Fedha Endelevu.

Oktoba Mosi, 2024 Baraza la Utawala litakutana kupitia ripoti kutoka Kamati Ndogo na kutoa mwongozo wa kimkakati, ikiwa ni pamoja na kushughulikia masuala ya kiutendaji ya CISNA.

Aidha, Oktoba Mosi na 2,024 wawakilishi kutoka mamlaka za wanachama watakusanyika kupokea ripoti kuhusu maendeleo ya CISNA na, inatakapohitajika watapitisha maazimio.

Oktoba 3 hadi 4,2024 utakuwa mkutano wa pamoja ambao utakuwa wazi kwa wafanyakazi wote kutoka mamlaka za nchi wanachama na washirika na utajumuisha vikao vya kujenga uwezo kuhusu mada mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news