Mongella akutana na wajumbe Halmashauri Kuu ya CCM Shinyanga

SHINYANGA-Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, Septemba 6, 2024 amekutana na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, wajumbe wa baraza la jumuiya, na mabalozi katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM pamoja na viongozi wa serikali, akiwemo wakuu wa idara wa Manispaa ya Shinyanga.
Mongella ameanza ziara ya siku saba mkoani Shinyanga kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2024 na kuimarisha uhai wa chama. Katika ziara hiyo, atafanya mikutano ya hadhara na ya ndani ili kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Shinyanga.

Ziara hiyo itamfikisha katika maeneo ya Shinyanga Vijijini, Kahama, Msalala, Kishapu, na Ushetu, ambako atakutana na viongozi wa chama na wananchi kujadili namna bora ya kuimarisha utekelezaji wa sera za chama kwa maendeleo ya mkoa.
Pia, ziara hii inalenga kuwahamasisha wanachama wa CCM kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama na kushughulikia kero za wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news