Mwekezaji mwenye mapato ya shilingi trilioni 160 kwa mwaka aonesha utayari Kabanga Nickel mkoani Kagera

PERTH-Waziri wa Madini,Mhe.Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Madini ya BHP inayotarajia kuingia ubia na Kampuni ya Lifezone Metal.
Ni kwa ajili ya kuwekeza nchini Tanzania katika mradi wa uchimbaji madini aina ya Nickel wilayani Ngara Mkoa wa Kagera.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kutoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa Kabanga Nickel unaosimamiwa na Kampuni ya ubia ya Tembo Nickel ambayo Serikali pia ni mwanahisa.
Mradi wa Kabanga Nickel unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 2.2 ambapo zaidi ya Dola Bilioni 1.6 zitatumika kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa mgodi na uchenjuaji wa madini utakaofanyika wilayani Ngara,Kagera.

Aidha,dola Milioni 600 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha usafishaji wa madini ambacho kitajengwa katika Ukanda Maalum wa Kiuchumi eneo la Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kampuni ya BHP ni moja kati ya kampuni kubwa tatu za madini duniani ambayo ina mapato dola Bilioni 60 kwa mwaka sawa na shilingi trilioni 160 kwa mwaka.

Kampuni ya BHP inayotarajiwa kuingia makubaliano ya ubia na kampuni ya Life Metals kuendeleza mradi wa Kabanga, ilifunga shughuli za uchimbaji madini barani Afrika miaka 15 iliyopita na sasa wapo tayari kurejea Afrika kupitia nchi ya Tanzania.
Waziri Mavunde alitumia fursa hiyo kuwashukuru kwa kuiamini Tanzania na kuamua kurudi kuwekeza kupitia mradi wa Kabanga.

Pia, amewahakikishia kwamba ni maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuwavutia wawekezaji kwa kutengeneza mazingira wezeshi ambayo yamejengwa kwa weledi kupitia falsafa yake ya 4R.
Aidha,Waziri Mavunde ambaye aliongozana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Japan ambaye pia anasimamia Australia,Baraka Luvanda Balozi ametembelea kujionea teknolojia itakayotumiwa kwenye ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini.
Kiwanda ambacho kitatumia teknolojia ya kisasa ya Hydrometallurgy kupitia Kampuni ya Tembo Nickel inayomiliki mgodi wa Kabanga Nickel uliopo Ngara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news