Naibu Waziri Pinda aagiza eneo mradi wa maji Usenya-Majimoto kupatiwa hati

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM Mlele

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amemuelekeza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Katavi kuhakikisha eneo la mradi wa maji safi kutoka Majimoto kwenda Usevya linapatiwa hati milki ndani ya wiki mbili.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Godfrey Mnzava akikagua mradi wa maji wa Majimoto-Usevya katika Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wakati wa kukagua miradi ya maendeleo leo Septemba 9,2024. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe. Geophrey Pinda.

Mhe. Pinda ametoa kauli hiyo leo Septemba 9, 2024 wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanywa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava katika Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Godfrey Mzava akizindua mradi wa maji wa Majimoto -Usevya ukiopo halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavvi tarehe 9 Sept 2024. Kulia ni Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda.

Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi mbio zake leo katika mkoa wa Katavi ambapo ulikabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hozza Mrindoko na mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe. Geophrey Pinda akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru mara baada ya kupokelewa mkoani Katavi katika Kijiji cha Mirumba Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele leo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Godfrey Mnzava akisisitiza jambo wakati akipata taarifa ya Lishe katika kijiji cha Kasansa halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 9 Sept 2024. Kulia ni Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda.

Amesema, wizara yake imekuwa ikisisitiza mara kwa mara maeneo yote yakiwemo ya umma kumilikishwa kwa hati hivyo ni lazima eneo hilo la mradi wa maji wa Majimoto -Usevya lipatiwe hati ndani ya wiki mbili.

Kauli ya mhe. Pinda inafuatia maelezo kuwa, mradi huo umeshindwa kuendeleza sehemu ya eneo lake kutokana na kutokuwa na hati milki ya eneo hilo jambo lililomshangaza kiongozi wa mbio za Mwenge Godftey Mnzava.

"Kiongozi wa mbio za mwenge kufuatia suala hili namuelekeza Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Katavi kuhakikisha eneo hili linapatiwa hati milki ya ardhi ndani ya wiki mbili,"amesema Mheshimiwa Pinda.
Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akipanda mti katika Shule ya Sekondari Mizengo Pinda wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo miradi ya Klabu za Mazingira, Dawa za Kulevya na Mapambano dhidi ya Rushwa ambayo imezinduliwa leo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Godfrey Mnzava amesisitiza kuwa, maeneo yote ya umma yamilikishwe kwa hati ili kuondoa mkanganyiko unaoweza kujitokeza na kama mwananchi ataamua kutoa eneo lake kwa umma basi taratibu zote za kumilikishwa kwa hati zifanyike.

"Tunasisitiza maeneo yote ya taasisi yapate milki ambayo ni hati ili kuondoa "confusion' zinazotokea, pale mwamanchi anapoamua kutoa sadaka eneo lake kwa umma na baada ya serikali kulitwaa kinachofuata ni umiliki na lazima utaratibu ufike mwisho wa kupata hati," amesema Mnzava.

Mradi wa maji safi kutoka Majimoto kwenda Usevya unatekelezwa kwa fedha za Programu ya Lipa kwa Matokeo ( Payment for Results PloR) kwa mikataba mitano yenye jumla ya ya kiasi cha shilingi bilioni 4.3.
Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akisalimiana na kiongozi wa mbio za Mwenge, Godfrey Mnzava mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili Kijiji cha Mirumba kilichopo Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi leo. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Mradi huo umekusudia kuboresha upatikanaji maji safi na salama katika vijiji vya Usevya, Msadya, Nyambwe, Ikuba na Minyoso kutoka skimu ya Majimogo na wakazi wapatao 34,650 watanufaika na mradi huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news