Naibu Waziri Sangu aitaka eGA kuwauza vijana wabunifu wa TEHAMA

NA LUSUNGU HELELA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kushiriki kwenye maonesho mbalimbali ya ubunifu ili kuonesha uzuri wa mifumo iliyobuniwa pamoja na umahiri wa vijana walioandaliwa na taasisi hiyo, ili vijana hao waweze kupata soko kwenye sekta binafsi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao,Mhandisi Benedict Ndomba pamoja na timu ya Menejimenti mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufunga mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi 65 wa Vyuo Vikuu mbalimbali yaliyofanyika kwa kipindi cha muda wa wiki 10 katika Kituo cha Ubunifu na Utafiti cha eGA kilichopo jijini Dodoma.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akifunga mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi 65 wa Vyuo Vikuu mbalimbali yaliyofanyika kwa kipindi cha muda wa wiki 10 katika Kituo cha Ubunifu na Utafiti cha eGA kilichopo jijini Dodoma.

Ameitaka eGA kutekeleza programu hiyo ya kukuza ubunifu katika TEHAMA kwa wanafunzi wa elimu ya juu kimkakati kwa kuwakutanisha vijana hao na waajiri ambao ni sekta binafsi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhr.Deus Sangi akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi 65 wa Vyuo Vikuu mbalimbali yaliyofanyika kwa kipindi cha muda wa wiki kumi katika Kituo cha Ubunifu na Utafiti cha eGA kilichopo jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Mhandisi Benedict Ndomba wakati akifunga mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi 65 wa Vyuo Vikuu yaliyofanyika kwa kipindi cha muda wa wiki kumi katika Kituo cha Ubunifu na Utafiti cha eGA kilichopo jijini Dodoma.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe.Sangu ameitaka eGA kuimarisha ushirikiano zaidi na Sekta binafsi ili vijana wanaoandaliwa na Taasisi hiyo waweze kukidhi hitaji la soko la ndani na nje ya nchi katika eneo la Tehama bunifu.

"Nimefarijika kusikia Benki ya NMB pamoja na Kampuni ya Vodacom ni miongoni mwa washirika wenu ambao mnashirikiana nao kwa kuwaeleza mahitaji ya soko na hivyo kuisaidia jinsi ya kuwapika vijana ili waendane na hitaji la soko.
Sehemu ya baadhi ya wanafunzi wakimsikliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu waliopatiwa mafunzo katika Kituo cha Ubunifu na Utafiti cha eGA kilichopo jijini Dodoma.

"Nimeambiwa mwaka jana Benki ya NMB ilichukua jumla ya vijana nane mliowaandaa, hii ni habari njema sana kwetu kama Serikali."

Katika hatua nyingine, Mhe.Sangu ameitaka eGA kuandaa kanzidata kwa vijana wote wanaopata mafunzo kwa vitendo katika Kituo hicho badala ya kuwaacha tu bila ya kuwa na taarifa zao.

Amesema ili kuhakikisha TEHAMA inatoa matokeo tarajiwa kwa Uchumi wa nchi ya Tanzania vijana hao wanadiwe kwa bunifu zao wanazofanya Ili kuweza kuwashawishi waajiri.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Eng. Benedict Ndomba akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sanga kwa ajili ta kufunga mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi 65 wa Vyuo Vikuu mbalimbali yaliyofanyika kwa kipindi cha muda wa wiki kumi katika Kituo cha Ubunifu na Utafiti cha eGA kilichopo jijini Dodoma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Eng. Benedict Ndomba amesema kuwa Kituo hicho kimekuwa kikifanya tafiti katika maeneo yote ya TEHAMA kwani tafiti hizo na bunifu zinaiweka nchi katika nafasi nzuri ya kushindana kwenye Uchumi wa kidijitali na Mataifa mengine.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu akiwa kwenye picha pamoja na Wanafunzi 65 wa Vyuo Vikuu mbalimbali wakati akifunga mafunzo kwa vitendo yaliyofanyika kwa kipindi cha muda wa wiki kumi katika Kituo cha Ubunifu na Utafiti cha eGA kilichopo jijini Dodoma.

Naye, Jane Claud ambaye ni mwanafunzi aliyepata mafunzo kwa vitendo katika Kituo hicho licha ya kushukuru kwa kupata fursa hiyo ameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa kituo kikubwa ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia yanatokea duniani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news