Naibu Waziri Sangu atoa salamu za pole kwa Afisa Ugavi mkoani Tabora

TABORA-Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Uyui mkoani Tabora amefika nyumbani kwa Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Ashura Kangombe kwa ajili ya kutoa pole kufuatia msiba wa Mama yake mzazi wa mtumishi huyo.
Mhe.Sangu amefika nyumbani hapo leo Jumamosi Septemba 21, 2024 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wabunge wenyeji wa eneo hilo.
Akizungumza katika msiba huo, Mhe.Sangu amesema, "Nimekuja Uyui kwa ajili ya kuzungumza na Watumishi wa Wilaya ya Uyui nikiwa njiani nimeambiwa Bi.Asha Kangombe kafiwa, Mimi nikiwa Mtumishi wa Watumishi nimekuja kumpa pole kwani asingepatwa na msiba huo angeshiriki kikao changu cha kuzungumza na watumishi wa Uyui."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news