NA LUSUNGU HELELA
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu amezielekeza Halmashauri Mkoani Tabora kutoa kipaumbele kwa vikundi vya akiba na mikopo vinavyoundwa na walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika utoaji wa mikopo.

Amesema vikundi hivyo vinastahili kupewa mikopo kwa kuwa vimepewa elimu ya ujasiriamali kupitia TASAF na vimehakikishwa kuwa na nidhamu katika ukopaji na ulipaji.
Amefafanua kuwa,mikopo ya asilimia kumi ambayo hutolewa na Halmashauri kote nchini huku akizitaka Halmasjauri hizo zifanye kazi kwa kushirikiana na TASAF ili zijifunze jinsi ilivyofanikiwa katika suala la utoaji mikopo kwa vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana.
Amesema,TASAF inasaidia walengwa wake kuanzisha na kuendesha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana na kufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ii kukuza uchumi wa kaya zao.

Hata hivyo, Mhe. Sangu amepiga marufuku utaratibu wa kazi za ajira za muda kwa makundi yafuatato ikiwemo wazee wenye zaidi ya miaka 65 na kuendelea, watoto chini ya miaka 18 na akina mama wajawazito pamoja na watu wenye ulemavu.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Chacha amesema ujio wa TASAF katika Mkoa wake imeleta mapinduzi makubwa kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi ambapo wanufaika 13,467 wamewezeshwa kujiunga na Bima ya Afya Iliyoboreshwa (CHF), kuboresha makazi na kuanzisha vikundi vya kukopeshana.