Ni upendo usiopimika, asanteni Ruvuma-Rais Dkt.Samia

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameshukuru kwa upendo aliopewa na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma, ambao wamejitokeza katika maeneo mbalimbali aliyotembelea mkoani humo alipokuwa katika ziara ya siku sita ya kikazi.
Ametoa shukurani hizo wakati akihutubia wananchi katika uwanja wa Majimaji, uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

"Ninawasgukuru sana wana Ruvuma kwa mapokezi mazuri sana na kwa ukarimu wenu kwangu,nimepata mapokezi makubwa katika kila eneo nililotembelea, wananchi walikuwa na furaha sana na wamenipa zawadi nyingi sana kuashiria kwamba wanatambua jitihada zetu za kuboresha maisha na ustawi wao.
"Wananchi wa Ruvuma asanteni sana, waheshimiwa wananchi ninaushukuru uongozi wa mkoa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Kanali Ahmed Abbas na sekretarieti yake kwa maandalizi na uratibu mzuri sana wa ziara hii.
"Shukurani hizo ziende pia kwa wakuu wa wilaya, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakurugenzi wa halmashauri, wabunge, madiwani na viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi zote, mkoa na wilaya zote.

"Ninawashukuru pia viongozi wa dini kwa maombi kila pahali tulipokuwa, walikuwepo na walituombea sana,ninawashukuru madereva wetu kwa muda wote wa siku sita, ziara imekwenda vema na hakuna lililotokea.Ninawashukuru vijana wa Skaunti na Vijana wa Hamasa,"

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news