PWANI-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani amepokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya hospitali ya Msoga na madawati 120 kwa ajili ya shule za msingi mbili za Chalinze.


