Orodha ya wateule wa EJAT 2023

DAR-(Septemba 19, 2024)-Majaji saba wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) wamehitimisha kazi ya kutathmini ubora na weledi wa kazi zipatazo 1,135 na kuwateua waandishi wa habari 72 watakaoingia katika kinyang’anyiro cha kumtambua mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu na mshindi wa jumla.
Kati ya waandishi wa habari 72, wanaume ni 45 (sawa na 62.5%) na wanawake 27 (sawa na 37.5%). Kati ya wateule hao, wateule 14 (19%) wanatoka katika runinga; 13 (18%) wanatoka vyombo vya mtandaoni, redio 20 (28%) na wateule 25 (35%) wanatoka kwenye magazeti.

Wateule wamepatikana kwa kukidhi vigezo vya ubora ambavyo ni pamoja na ukweli, usahihi, uanuai, haki, kina, utafiti, ubunifu, uvumbuzi, upekee, uchambuzi, uwajibikaji, ufichuaji maovu, uadilifu, uwasilishaji unaoeleweka na uchunguzi. Ifahamike pia kwamba vigezo maalum vilitumika kuzingatia aina tofauti ya vyombo vya habari kama vile redio, televisheni, magazeti na habari za mitandaoni.

Kabla ya kutaja majina ya wateule hao 72 ni muhimu ifahamike kwamba kinyang’anyiro cha kumtambua mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu na mshindi wa jumla kwa makundi 20 ya kushindaniwa kitakuwa siku ya jumamosi, tarehe 28 Septemba, 2024 ambapo mgeni rasmi katika siku ya kilele cha kinyang’anyiro atakuwa ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Mabunge Duniani, Dkt Tulia Akson.

Mgeni rasmi ndiye atakayemkabidhi tuzo mshindi wa jumla atakayewapiku kwa umahiri waandishi wengine 71 katika hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Aga Khan Daimond Jubilee, Dar es Salaam. Hii itakuwa ni mara ya 15 kutoa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania.

Moja ya jambo la kipekee katika kilele cha kinyang’anyiro hicho ni pamoja na kusikia kutoka kwa jopo la majaji kuhusu viwango vya uandishi wa habari za magazeti, redio, televisheni na mitandaoni kwa habari zilizohusu uwekezaji wa kampuni ya DP world katika bandari za Tanzania, habari kuhusu Ngorongoro na wamasai na kuhusu maporomoko ya Hanang.

Jambo la pili la kipekee ni kumshuhudia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry Silaa akizindua Jarida la Tuzo na Tuzo magazine ambayo yanajikita kuhamasisha umahiri katika sekta mbalimbali Tanzania na nje ya Tanzania. Kwa kuanzia majarida hayo, moja la Kiswahili na lingine la Kiingereza yatabeba maudhui ya tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania (EJAT).

Moja ya maudhui katika majarida yote mawili ni simulizi ya maisha ya wateule wote. Kazi ya kuandika simulizi hizo inaanza leo, hivyo wateule wote wawe tayari kufikiwa na waandishi wa Jarida la Tuzo wakati wowote kuanzia sasa. Maudhui mengine ni ya wafadhili wa tuzo ambao simulizi zitahusu mchango wao katika kubadilisha maisha ya watu ikiwemo kukuza na kujenga tasnia ya habari.

Aidha ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza kazi za kihabari kwa EJAT 2023 zimeongezeka hadi 1,135 kutoka kazi 893 za EJAT 2022. EJAT 2020 kazi zilikuwa 396 na EJAT 2021 kazi zilikuwa 608.

Waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka huu waliongoza kwa kuwasilisha kazi 290, wakifuatiwa na mkoa wa Arusha uliokuwa na kazi 81, Mwanza kazi 74, Iringa ilishika nafasi ya nne kwa kuwa na kazi 72, wakati mkoa wa Mtwara ulishika nafasi ya tano kwa kuwa na kazi 49. Kwa upande wa Zanzibar, kazi zilizopokelewa ni kutoka Kaskazini Pemba (36) Pemba Kusini (43) na Mjini Magharibi (29).

Dirisha la kupokea kazi za waandishi wa habari lilifunguliwa tangu Novemba 15, mwaka jana na kufungwa Februari 28, mwaka huu. Kazi ya kuchambua na kutathmini ubora wa kazi za kihabari za mwaka 2023 ilianza tarehe 7 hadi 15 baada ya Naibu msajili wa mahakama kuu, Morogoro, Mheshimiwa Fadhil Mbelwa kuwaapisha majaji.

Jopo la Majaji liliongozwa na Halima Shariff, katibu wake Dkt Egbert Mkoko na majaji wengine wakiwa ni pamoja na Ndugu Mkumbwa Ally, Eshe Muhiddin, Jeniffer Sumi, Halima Msellemu na Absalom Kibanda.

Jopo lilichaguliwa na wakuu wa taasisi za kihabari zinazounda kamati ya maandalizi ya EJAT kwa kuzingatia uadilifu, ujuzi na uzoefu katika uandishi wa habari, uwezo wa kuchambua na kutoa tathmini sahihi, uelewa wa mabadiliko ya kidigitali, uzoefu wa kimataifa au wa kijamii.

Aidha, jopo la majaji lilizingatia uwiano wa kizazi kipya na cha zamani, waliopo kazini na waliostaafu, wabobezi wa maudhui mahsusi, usawa wa kijinsia, uwakilishi wa Zanzibar na Tanzania Bara na uwakilishi wa aina ya vyombo vya habari (magazeti, redio, luninga na mitandao).

Mbali na Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari, mchakato wa kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio Katika Uandishi wa Habari (LAJA) 2024 unatarajiwa kuhitimishwa leo na wakuu wa kamati ya maandalizi. Tuzo hii humtambua mwandishi ambaye katika maisha yake ametoa mchango mkubwa katika kuiendeleza tasnia ya habari.

Taasisi zinaounda Kamati ya Maandalizi ni Wakfu wa Vyombo vya Habari (TMF), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), HakiElimu, Umoja wa Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Sikika, Misa – Tan na Twaweza.

Sasa nimalizie kwa kusoma orodha ya wateule wa EJAT 2023 pamoja na vyombo vyao:

 

NA.JINAJINSIACHOMBOMKOA
1Thomas Masalu LunyaloMMazingira FMMara
2Abdallah Bakari NassoroMNipasheMtwara
3Jacob Mogesi MusendaMThe CitizenDar es Salaam
4Marco MaduhuMShinyanga Press ClubShinyanga
5Salum Vuai IssaMZanzibar LeoZanzibar
6Jackline Victor KuwandaFThe ChanzoDodoma
7Stanslaus LambertMSwahili 360Dar es Salaam
8Zacharia NyamogaMIPC Mkombozi TVIringa
9Irene MwakalingaFTBC1Iringa
10Said Ally SindoMStorm FMGeita
11Joshua StephenMNuktaDar es Salaam
12Samweli MpogoleMHighlands FMMbeya
13Shekha SuleimanFZBCPemba
14Abel KilumbuMDar 24Dar es Salaam
15Khamis MohamedMZanzibar LeoZanzibar
16Abdiel Jumanne SiffiMUFMDar es Salaam
17Julius Maricha MarichaMThe CitizenDar es Salaam
18Eliya SolomonMMwanaspotiDar es Salaam
19Huwaida Nassor Moh’dFAs Salaam FMZanzibar
20Rehema Evance MwaikemaFUTVSimiyu
21Philip Mwihava MwihavaMClouds FMDar es Salaam
22Zourha John MalisaFMwananchiDar es Salaam
23Linus Ananias GamarwaMTBCDodoma
24Catherine SekibahaFPangani FMPangani Tanga
25Herieth MakwettaFMwananchiDar es Salaam
26George HelahelaMMwananchiDar es Salaam
27Esau Ezra Ng’umbiMNukta HabariDar es Salaam
28Benson Eustace JacobMUTVKagera
290Mariamu Ally AbdallahFPangani FMTanga
30Adam Gabriel HhandoMCG FMTabora
31Sanula Renatus AthanasMNipasheDar es Salaam
32Elizabeth Edward KusekwaFMwananchiDar es Salaam
33Pamela Nasphory ChilongolaFMwananchiDar es Salaam
34Rodgers SimonMITVDar es Salaam
35Mukrim Mohamed KhamisMKTV TZ OnlineZanzibar
36Ephrahem Edward BahemuMMwananchiDar es Salaam
37Mkwaji Reuben MasatuFUTVDar es Salaam
38Lukelo Francis HauleMThe ChanzoDar es Salaam
39Benjamin MzingaMITVDar es Salaam
40Dickson Shukran KanyikaMRFANjombe
41Hamisi Makungu HamisiMPangani FMPangani Tanga
42Halfan ChusiMNipasheDar es Salaam
43Kelvin Paul MatandikoMMwananchiDar es Salaam
44Waryoba Musa WaryobaMMontessory TanzaniaMwanza
45Anna Peter  MbuthuFTBCArusha
46Egan SallaMBBCDar es Salaam
47Imma Rashid MbuguniMMajira OnlineDar es Salaam
48Haika E. KimaroFThe CitizenMtwara
49Margareth Msafiri GeddyMTBC SafariDar es Salaam
50Yohana Chance ChalleMMwanaspotiMbeya
51Mgongo Kaitira MafuruMMwananchiMwanza
52Mercy Yasin MbayaFUTVDar es Salaam
53Imani Raphael MakongoroFMwananchiPwani
54Fatma Abdallah ChikaweFUTVDar es Salaam
55Brown Benny MbwawaMWasafi FMMbeya
56Ayoub Stanley NyondoMShamba FMIringa
57Warioba Igombe WariobaMUhuruMara
58Salome Gregory SumbyaFThe CitizenDar es Salaam
59Veronica Natalis MatabaFDW SwahiliArusha
60Saa Mbwana ZumoFPangani FMPangani Tanga
61Said Ali NgambaMUyui FMTabora
62Lugendo MadegeMUFMDar es Salaam
63Anna PotinusFMwananchiMwanza
64Christina MwakangaleFNipasheDar es Salaam
65Rauhiya M ShabanFBomba FMZanzibar
66Hazla Omary QuireFThe Tanzania TimesArusha
67Lucy Patrick SamsonFNuktaDar es Salaam
68Mohamed Hammie RajabuMHabari LeoDar es Salaam
69Amina Deogratias SemagogwaFRadio KwizeraKigoma
70Hellen Nachilongo MkisiFThe CitizenDar es Salaam
71Alfred Bulahya JakubaMDodoma FMDodoma
72Waziri Iddi SukaMTumaini TVDar es Salaam

Hongereni sana kuingia katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2023.

Ernest S. Sungura

Mwenyekiti

Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2023




Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news