Polisi abisha hodi nyumba kwa nyumba kusisitiza malezi bora kwa watoto

MARA-Polisi Kata wa Kata ya Kisangura Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Genuine Kimario ameanzisha kampeni maalumu ya nyumba kwa nyumba inayolenga kuwahimiza wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa malezi bora kwa watoto.
Katika kampeni hii, Kimario anawatembelea wazazi na walezi majumbani mwao, akitoa elimu kuhusu umuhimu wa malezi bora kama njia ya kudhibiti vitendo vya uhalifu.

Aidha,kampeni hii inatarajiwa kuwafikia wazazi na walezi wengi zaidi katika kata hiyo, huku ikiendeshwa kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji, walimu, na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na haki za watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news