ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendeleza juhudi za kuimarisha michezo kwa lengo la kuinua vipaji vya vijana.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amelitaka Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kuendelea kuimarisha michuano hiyo ambayo sasa imekuwa na sura ya kitaifa na kuunga mkono kila mwaka.
Katika mchezo huo wa Fainali timu ya Ponchink City imeibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuwa mabingwa wapya wa Yamle Yamle.
Halikadhalika, Dkt.Mwinyi ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kuendelea kuwa wadhamini wakuu wa michuano hiyo.