Profesa Mwegoha abainisha Mzumbe walivyojikita kutoa kozi ya Tathmini na Ufuatiliaji

ZANZIBAR-Makamu Mkuu wa Chuo wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema Mzumbe imejitanabaisha kama taasisi ya elimu ya juu inayojikita katika kutoa kozi ya Tathmini na Ufuatiliaji katika ngazi ya Shahada za Awali za Umahiri ili kuwa na wataalamu watakaolisaidia taifa katika shughuli za maendeleo na kukua kwa uchumi.
Prof. Mwegoha ameyasema hayo leo Zanzibar akiwa ni mtoa mada elekezi katika Kongamano la Tatu la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji, Tathimini na Kujifunza linaloendelea katika Hoteli ya Golden Tulip ambapo Chuo Kikuu Mzumbe kinashiriki kama sehemu ya waratibu wa Mkutano huo, watoa mada na wanajopo katika baadhi ya mada zinazowasilishwa.

Prof. Mwegoha amesema Taasisi za Elimu ya Juu zina wajibu wa kuendelea kuzalisha wataalamu na wabobevu wa Kada ya Tathimini na Ufuatiliaji wa kwakuwa ni hitaji la kimkakati kwa sasa.
“Katika ulimwengu wa sasa, teknolojia inaimarisha ufuatiliaji na tathmini kwa kusaidia ukusanyaji wa taarifa, uchambuzi na kuandaa taarifa zinazopelekea kufanya maamuzi sahihi. Hivyo uwezo wa kufanikisha haya mbali ya teknolojia unahitaji kada maalumu ya wataalamu waliofunzwa kutumia nyenzo hizo kwa ufanisi,” Prof. Mwegoha amesisitiza.

Aidha Prof. Mwegoha amefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Mzumbe kipo mstari wa mbele katika kutoa mafunzo ya muda mrefu (Shahada ya Awali na Shahada ya Umahili) Pamoja na mafunzo ya muda mfupi katika taaluma ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa ajili ya wataalamu watakaoweza kusimamia masuala ya ufuatiliaji na tathmini ili kusimamia kikamilifu miradi na programu za maendeleo kutokana na taarifa zinazokusanywa, kuchambuliwa na kutumiwa kwa usahihi ili kuleta maendeleo kwa sekta za Umma / Binafsi na Taifa kwa ujumla.
“Dhamira yetu ni kuandaa wahitimu ambao wanaweza kutoa mchango mkubwa katika mipango ya sekta za umma na binafsi. Taasisi za elimu ya juu ni vituo vya utafiti na uvumbuzi, tumejikita hapo," amesisitiza Prof. Mwegoha.

Katika wasilisho lake Prof. Mwegoha amesema kuwa Mzumbe ni Chuo cha kwanza kuanzisha programu ya umahiri katika Ufuatiliaji na Tathmini nchini Tanzania. Huku akieleza kuwa hatua hiyo ni matokeo ya msukumo wa uhitaji wa taaluma hiyo katika shughuli za maendeleo.

Aidha, Chuo hicho kimejikita katika kufundisha na kufanya utafiti katika fani ya Ufuatiliaji na Tathmini, shughuli ambayo inaratibiwa vizuri na wahadhiri pamoja na wanafunzi wa Shahada ya Umahiri wa kozi hiyo tangu 2015, ambapo matokeo ya uvumbuzi na tafiti hizo yamekua yalichapishwa kupitia Jarida la Afrika Mashariki la Ufuatiliaji na Tathmini.
Amebainisha kuwa, Vyuo vikuu vina jukumu la kutoa elimu, kufanya utafiti na kujenga msingi thabiti ya kufanya tathmini na ufuatiliaji ambao uleta matokeo chanya katika kusimamia uendeshaji na usimamizi wa miradi katika sekta ya umma na binafsi nchini.
Kongamano la Tatu la Wiki ya Ufuatiliaji, Tathimini na Kujifunza linafanyika katika Hotel ya Golden Tulip Zanzibar limefunguliwa na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Abdulla na linashirikisha washiriki takribani 650 kutoka mataifa zaidi ya 13.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news