Prof.Makubi awauma sikio watumishi Hospitali ya Benjamin Mkapa

DODOMA-Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa amekutana na baadhi ya watumishi wa mapokezi, usajili wagonjwa, wahudumu, maafisa huduma bora kwa wateja na wahasibu.
"Nimewaita hapa ili tuelewane katika baadhi ya mambo ya kubadilika kifikra na tabia na kuipeleka BMH katika hatua nyingine, kwanza , kubadili lugha zetu.

"Tumjali mgonjwa na kumuhudumia kwa haraka, kubadilika kwenu kunapaswa kuanzie moyoni kwa utashi na matendo na hapa nazungumzia kuanzia walinzi mpaka wakurugenzi," amesema Prof. Makubi na kukumbushia kuwa suala la ubora wa huduma kwa Wateja ndo kipaumbele kwa BMH.

Ameongeza kuwa wataalamu wa afya wamefundishwa uwajibikaji wa hali ya juu na unapokuwa katika eneo lako kuwa mtu wa kutatua changamoto kwa haraka . Hii hali itatokea tu kama nyie watumishi mtaonyesha sense of ownership, uzalendo na uwajibikaji toka moyoni.

"Kila tunapoona kuna jambo halijakaa sawa usisubiri kiongozi ajekutatua wewe mwenyewe tatua ikishindikana toa taarifa kwa viongozi," amesema Prof. Makubi.

Kwa upande wake Frank Mathayo muuguzi amewasihi watumishi wenzake kuwa na moyo wa uvumilivu wakati wanapotoa huduma

"Nitoe mfano siku moja mgonjwa aliniambia muwe mnatuvumilia maana mtamuona mgonjwa mmoja alie letwa lakini nataka nikuambie hata aliye mleta mgonjwa ni mgonjwa zaidi tena huenda amekata tamaa, hii ilinifanya niongeze upendo kwa wagonjwa hivyo nanyi watumishi wenzangu nawaomba tuwe wa vumilivu tunapo wahudumia wagonjwa,"amesema Mathayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa,Prof. Abel Makubi ameendelea kukutana na watumishi mbalimbali ndani ya BMH ili kuwajengea uelewa wa pamoja katika kutekeleza majukumu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news