Rais Azali Assoumani achomwa kisu

MORONI-Afisa mmoja wa Jeshi la Polisi nchini Comoro anashikiliwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa tuhuma za kumshambulia Rais Azali Assoumani kwa kisu, ni baada ya kwenda kutoa rambirambi zake kwa familia ya shehe mmoja katika mji wa Salimani katikati ya kisiwa cha Ngazija.

Tukio hilo limetokea Septemba 13,2024 ambapo Msemaji wa Serikali,Fatima Ahamada aliieleza Reuters kuwa, "Rais Azali Assoumani alijeruhiwa kidogo kwa kisu wakati wa mazishi ya shehe maarufu hapa nchini. Majeraha yake si makubwa na amerejea nyumbani."

Licha ya hali ngumu ya kiuchumi inayowakabili wananchi nchini humo, Rais Assoumani anatuhumiwa kufanya upendeleo katia uongozi wake ambapo Julai, mwaka huu alimteua mtoto wake Nour El Fath kuwa msimamizi na mratibu wa masuala ya Serikali.

Rais Assoumani mwenye umri wa miaka 65 mtawala wa zamani wa kijeshi alichukua madaraka kupitia mapinduzi 1999, na kurudi tena Februari 21, 2016.

Aidha,alibadilisha katiba na kuchaguliwa kwa mhula wa tatu Januari,2024 baada ya uchaguzi ulozusha upinzani mkubwa na ghasia za siku mbili.

Vilevile,wapinzani wamekuwa wakidai kwamba tume ya uchaguzi inakipendelea chama tawala, madai ambayo tume hiyo imekuwa ikiyakanusha na imeeleza kuwa uchaguzi unafanyika kwa njia ya uwazi na haki.
Rais Azali Assoumani. (PICHA NA MENAFN).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news