BALI-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema,Zanzibar ina nafasi nzuri ya kujifunza mambo mbalimbali kikiwemo kilimo na usarifu wa mwani, uchimbaji mafuta na gesi, utalii, na bandari kwa Indonesia.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 1,2024 alipofungua Jukwaa la Uwekezaji la Zanzibar-Indonesia 2024, ambalo limeandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) katika Hoteli ya Sofitel jijini Bali, Indonesia.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kufurahishwa na muamko wa jukwaa hilo kwa kujitokeza kwa wingi wawekezaji ambao wameonesha nia ya kuwekeza Tanzania, ikiwemo Zanzibar.
Hivyo,Watanzania watarajie wawekezaji mbalimbali, hususan katika sekta ya Uchumi wa Buluu kutoka Indonesia.