BALI-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amelipongeza na kulishukuru Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Indonesia (Indonesian Aid) kwa ufadhili wa programu mbalimbali za kuwajengea uwezo Watanzania katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amemfahamisha Bw. Tormarbulang kuhusu dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushirikiana na Shirika hilo katika utekelezaji wa programu mbalimbali zenye manufaa na tija kwa wananchi wa Zanzibar na kumshawishi kwa kuangalia uwezekano wa kufadhili programu za kuwajengea uwezo walengwa.
Bw. Tormarbulang Tobing amekubali ombi la Rais Dkt. Mwinyi na kumhakikishia utayari wake wa kuimarisha ushirikiano na Zanzibar.