Rais Dkt.Mwinyi arejea Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk.Hussein Ali Mwinyi leo Septemba 8,2024 amerejea Zanzibar, baada ya kumaliza ziara yake nchini Indonesia na kushiriki katika Sherehe za Miaka 50 ya siku ya Ushindi nchini Msumbiji.
Dkt.Mwinyi amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe Hemed Suleiman Abdulla pamoja na viongozi wengine wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Vilevile Dkt. Mwinyi amepata fursa ya kuongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika ziara hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news