Rais Dkt.Mwinyi asisitiza maadili mema kwa vijana na watoto

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kutumia maadhimisho ya Kuzaliwa Mtume Muhamad (SAW) kuwafundisha maadili mema vijana na watoto.
Alhaji Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 28,2024 katika Masjid Ayytul Kisauni Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi alipojumuika katika sala ya Ijumaa.
Ameeleza kuwa, vitendo Viovu vinavyotokea katika jamii hivi sasa vinachangiwa kwa kiasi kikubwa kwa vijana kukosa maadili na tabia njema.

Alhaji Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa ni vyema majukwaa ya Maulid yakatumika kuwafundisha vijana na watoto kutekeleza maadili mema ya kiislamu ili kuwa na jamii Bora.
Aidha,amewasisitiza waumini wa dini ya kiislamu kudumisha Amani na Utulivu ili Serikali itekeleze mipango ya Maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news