Rais Dkt.Mwinyi atembelea kiwanda cha kusarifu majani ya karafuu na kutengeneza mafuta jijini Jakarta

JAKARTA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na ujumbe wake, ametembelea Kiwanda cha INDESSO cha kusarifu majani ya karafuu na kutengeneza mafuta kwa matumizi mbalimbali kama vile dawa na manukato, kilichopo Cileungsi jijini Jakarta, Indonesia.
Akiwa katika kiwanda hicho leo Septemba 5,2024, Rais Dkt.Mwinyi amejionea hatua mbalimbali za kusarifu majani ya karafuu pamoja na shughuli nyingine zinazofanywa na kiwanda hicho.

Akitoa maelezo mbele ya Rais Dkt.Mwinyi, Bw. Robby Gunawan ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho amesema kuwa, kiwanda hicho kimepiga hatua kubwa za mafanikio tangu kuanzishwa kwake Pemba mwaka 2019.
Ni kwa kujenga vinu nane vya kusarifu majani ya karafuu pamoja na kukuza uchumi kwa kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi wa Zanzibar kupitia vinu hivyo.

Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Mwinyi ameambatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Moshe Tembele, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Mhe. Saada Mkuya Salum,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Sharif Ali Sharif, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed,
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Mhe. Shaabani Ali Othman, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Cosato David Chumi pamoja na wakuu taasisi mbalimbali za SMZ na SMT.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news