Rais Dkt.Mwinyi ateta na uongozi wa Chuo cha Al Madrasatul Swiffati Nnabawiyyatil Karimah

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuhudhuria dua maalum siku Septemba 25, 2024 ya kuwaombea viongozi wa nchi iliyoandaliwa na Chuo cha Al Madrasatul Swiffati Nnabawiyyatil Karimah maarufu Msolopa cha Kilimani.
Dua hiyo itafanyika katika viwanja vya Chuo cha Al Madrasatul Swiffati Nnabawiyyatil Karimah maarufu Msolopa cha Kilimani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, itasomwa na chuo hicho kwa kushirikiana na Zawiyyah zote za mjini na vijijini.
Aidha, inatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya waumini wa Kiislam wapatao 5,000 kwa pamoja itawaombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Alhajj Dkt. Mwinyi kutokana na kazi kubwa wanazofanya ya kuleta maendeleo ya nchi.
Chuo cha Al Madrasatul Swiffati Nnabawiyyatil Karimah maarufu Msolopa cha Kilimani, kilianzishwa mwaka 1975 eneo la Jeshini Migombani na baadae mwaka 1976 kilihamia kilimani ambako hadi sasa ndio makao makuu ya chuo hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news