MAPUTO-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili jijini Maputo, Msumbiji akitokea nchini Indonesia kwa gwaride maalum na ujumbe wake akiwemo Mkewe Mama Mariam Mwinyi.

Kuhudhuria kwake katika sherehe hizo kunatokana na mualiko Maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi.