Rais Dkt.Mwinyi azindua Hoteli ya Shukran Palace, aendelea kuwakaribisha wawekezaji

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa, Serikali itaendelea na ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege, barabara, na bandari ili kuvutia wawekezaji zaidi kuja kuwekeza nchini.
Dkt. Mwinyi amefafanua kuwa Serikali inaendelea na mipango ya kuimarisha viwanja vya ndege, ikiwemo uwanja wa Pemba, ili kufungua milango zaidi kwa watalii na wawekezaji kuvutiwa kuja Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 21, 2024, alipofungua Hoteli ya Shukran Palace iliyopo Michamvi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza menejimenti ya Taasisi ya Nada Group Hotels kwa kuwekeza nchini kupitia mradi huo mkubwa na ameahidi kwamba Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha unafanikiwa.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ametaja maeneo mengine ya kipaumbele kuwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri, Bandari ya Malindi, Mangapwani, na Shumba kisiwani Pemba, huku akisisitiza wananchi kuunga mkono juhudi hizo.

Vilevile Rais Mwinyi amewahimiza wawekezaji kuweka mkazo zaidi kwenye kununua bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa ndani ili kuwainua kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news