Rais Dkt.Mwinyi katika Fainali ya Yamle Yamle leo

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili ndani ya Uwanja wa Gombani Pemba kushuhudia fainali ya kandanda kuwania Kombe la Yamle Yamle kati ya timu ya Ponchiki City na Wete City zote za Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 14 Septemba 2024.
Alipowasili Uwanja wa ndege Rais Dk.Mwinyi amepokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh.Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Mattar Zahor Masoud.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news