Rais Dkt.Mwinyi na ujumbe wake waelekea jijini Jakarta

BALI-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa anaendelea na ziara yake nchini Indonesia leo Septemba 4, 2024 ameondoka Bali kuelekea jijini Jakarta na ujumbe wake akiwemo mkewe, Mama Mariam Mwinyi.
Katika uwanja wa ndege wa Ngurah Rai, Bali Rais Dk.Mwinyi ameagwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje Indonesia, Balozi Acep Somantri pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Moshe Tembele.
Rais Dkt. Mwinyi alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Indonesia na Afrika 2024, ambao umehitimishwa Septemba 3, 2024, katika hoteli ya Mulia jijini Bali Indonesia.

Akiwa jijini Jakarta, Rais Dkt. Mwinyi atatembelea mashamba ya mwani, Kiwanda cha Kuchakata Mafuta ya Karafuu pamoja na Bandari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news