Rais Dkt.Samia aagiza vyombo vya uchunguzi kumpelekea taarifa ya kina kifo cha kiongozi wa CHADEMA

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameagiza vyombo vya uchunguzi kumpelekea taarifa ya mauaji ya Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mohamed Ali Kibao.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa leo Septemba 8,2024 kupitia kurasa zake rasmi z mitandao ya kijamii.

"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA, Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

"Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka.

"Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news