Rais Dkt.Samia asema yasiyofahamika kuhusu Hayati Sokoine

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, Serikali inatarajia kujenga Makumbusho ya Marais ambayo itajengwa katika eneo la hekari 50 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhiria uzinduzi wa Kitabu kuhusu Maisha na Uongozi wa Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977 mpaka 1980 na 1983 mpaka 1984 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Familia ya hayati Edward Moringe Sokoine baada ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Makamu wa Rais. Mhe. Philip Isdor Mpango Kitabu pamoja na Viongozi wengine waliohudhiria uzinduzi wa Kitabu kuhusu Maisha na Uongozi wa Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977 mpaka 1980 na 1983 mpaka 1984 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Familia ya hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Familia ya hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Familia ya hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.

Dkt.Samia ameyasema hayo leo Septemba 30,2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kitabu cha Edward Moringe Sokoine (Maisha na Uongozi Wake).

Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara mbili, tangu Februari 13,1977 hadi Novemba 7,1980 na mara ya pili kuanzia Februari 24, 1983 hadi Aprili 12,1984 alipofariki kutokana na ajali ya gari.

"Nataka nizungumzie pendekezo lililotolewa na Balozi Sokoine kwamba kuwe na kituo mahususi cha kuweka historia na kumbukumbu za viongozi, nataka nitoe taarifa kwamba pendekezo hili limeanza kufanyiwa kazi.
Muonekanao wa Kitabu cha Edward Moringe Sokoine (Maisha na Uongozi Wake).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wake wa hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.
"Kuna mradi wa Makumbusho ya Marais, mradi huu ni mradi namba 5221 eneo liko Mtumba na tumetenga shilingi bilioni 34 kwa ajili ya mradi huu na mwaka huu tumeanza kutenga bajeti ndogo kama bilioni moja na kitu na eneo lile lina ukubwa wa ekari 50 pale Dodoma, kwa hiyo hili tunalifanyia kazi."

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amesema, Hayati Sokoine alikuwa na sifa nyingi ambazo zinapaswa kuigwa na viongozi wa sasa na baadaye ikiwemo uaminifu kwa mamlaka ya uteuzi na wananchi.

Rais Dkt.Samia amesema kuwa,Hayati Sokoine alikuwa na sifa hiyo na akaaminiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika umri mdogo, hivyo ni funzo kwa wengine kuhusu uadilifu na uchapakazi kwa bidii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu kuhusu Maisha na Uongozi wa Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977 mpaka 1980 na 1983 mpaka 1984 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.

"Sokoine alikuwa mwaminifu sana kwa mamlaka yake ya uteuzi na kwa wananchi ndio maana haishangazi kwamba alikasimiwa majukumu mengi na makubwa ikiwemo Waziri Mkuu katika umri mdogo, katika hili tunajifunza kwamba ukiwa mwadilifu na mchapakazi hauna haja ya kukimbizana na vyeo bali vyeo vitakufuata ulipo.

“Vilevile Sokoine aliongoza vita dhidi ya uhujumu uchumi na madhara yake, japo alifariki kabla ya kuona matokeo yake, lakini dhamira yake ilikuwa wazi, funzo kubwa kabisa la uongozi kutoka kwa Sokoine ni uaminifu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mtoto wa hayati Edward Moringe Sokoine, Balozi Joseph Edward Sokoine kabla ya kuzindua Kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.

"Nidhamu na uchapakazi, na hii mimi pamoja na vijana wa leo tunatakiwa kujifunza hapa, sifa ambazo ningependa kuzisisitiza kwa viongozi wa sasa na baadaye.

Wakati huo huo, Rais Dkt.Samia amesema, Hayati Edward Moringe Sokoine alikuwa na uwezo mkubwa wa kutafuta majibu ya changanoto kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Pia, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametolea mfano wa pendekezo la kutumia punda kama chombo cha usafiri kwa maafisa wa serikali vijijini.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.

"Funzo jingine tunalolipata ni uongozi unaoacha alama. Alama za Hayati Sokoine zipo takribani katika kila sekta aliyopita, akiwa Waziri Mdogo yaani Naibu Waziri wa Mawasiliano,Uchukuzi na Kazi alisimamia kikamilifu ujenzi wa Reli ya TAZARA.

"Ambayo hivi sasa, karibuni nilipokuwa Beijing, kule China, nchi zetu tatu, Tanzania, Zambia na China tumeamua kukarabati reli hiyo na kuifanya ya kisasa."

Rais Dkt.Samia amesema, Reli ya TAZARA ilikuwa na mchango mkubwa katika vita ya ukombozi katika nchi za Kusini mwa Afrika.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.

"Na ni dhamira tetu,kuifufua ili itusaidie katika kutekeleza malengo ya Umoja wa Afrika, Ajenda 2063 yenye lengo la kuzifanya nchi za Afrika kufanya biashara kwa wepesi,alama nyingine ya kiuongozi tunaiona alipokuwa Waziri wa Ulinzi na JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) alishauri na ikaridhiwa wanawake waanze kuandikishwa jeshini.

"Hii isingetarajiwa kutoka kwa kijana aliyekulia kwenye jamii ya Kimasai,ambapo wakati ule nafasi ya mwanamke ilikuwa chini kabisa, lakini Sokoine hakutaka,"

Balozi Sokoine

Awali akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu, mtoto wa Hayati Edward Moringe Sokoine, Balozi Joseph Sokoine amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kutimiza ndoto ya miaka 40 ya kuandika kitabu cha historia ya baba yake.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.

"Miaka 40 ya kusoma kitabu cha maisha na mmoja wa viongozi wa Tanzania imetimia kwa msaada wako Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Ninakumbuka,nilipokea simu kutoka kwa msaidizi wa Makamu wa Rais,akihitaji kupitia taarifa za mzee (Hayati Edward Moringe Sokoine), nilimweleza nina kitabu cha hotuba aliyoitoa Oktoba 1982.

"Na nikamweleza kuna hotuba nyingine aliyoitoa Machi, 1983. Kwenye mkutano mkuu wa chama,na kwamba hotuba nyingine zinaweza kupatikana bungeni,niliahidi kumtumia kitabu hicho na nilifanya hivyo."

Pia, Balozi Sokoine amesema, baadaye alipokea simu nyingine kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Isdor Mpango akitaka kufahamu kama kuna jambo lingine ambalo Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa uhai wake aliandika.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.

Ameongeza, baada ya kumweleza Makamu wa Rais dhamira ya muda mrefu ya familia kutaka kuandika kitabu alimweleza, "baada ya maelezo yale alinieleza kuhusu umuhimu wa kuandika kitabu cha watu mashuhuri ili tusipoteze urithi na sehemu ya historia ya nchi yetu.

"Makamu wa Rais Dkt.Phili Isdor Mpango aliniamia nimuachie suala hilo na ataona cha kufanya,na kwamba angeliwasilisha kwako Mheshimiwa Rais (Dkt.Samia Suluhu Hassan)."

Amesema,baada ya Makamu wa Rais Dkt.Mpango kulifikisha suala hilo kwa Rais Dkt.Samia yalitolewa maelekezo na kazi ikaanza mara moja ndipo kikapatikana kitabu ambacho kimezinduliwa leo.

Waziri Simbachawene

Kwa upande wake,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameagiza viongozi wa umma kusoma kitabu hicho cha Hayati Edward Moringe Sokoine (Maisha na Uongozi Wake) ili wajifunze kuhusu utendaji bora wa kiongozi huyo wakati wa uhai wake.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Hayati Edward Moringe Sokoine kinachohusu Maisha na Uongozi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) leo tarehe 30 Septemba, 2024.

"Ninaomba niwasihi viongozi wote wa umma katika ngazi zote nchini, wakisome kitabu hiki na waendelee kudumisha uadilifu na uzalendo muda wote wanapokuwa ndani na nje ya utumishi wao.

"Kwa hakika, mtumishi mwadilifu ni rahisi sana kuonekana na kutambulika na ndiyo maana leo hii tunatambua uadilifu na uzalendo wa Hayati Sokoine pamoja na kwamba hayupo nasi takribani miaka 40."
Pia, Waziri Simbachawene amewashukuru wote walioandaa kitabu hicho ikiwemo Taasisi ya UONGOZI, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA),waandishi wa kitabu hicho, wahariri,wachapishaji, viongozi waliohojiwa na wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine.

"Kipekee kabisa ninaishukuru familia ya hayati Sokoine kwa kuruhusu maelezo ya kina kuhusu maisha na kazi ya hayati Sokoine kufikishwa kwa Watanzania na ulimwengu kwa ujumla.
"Pia, ninapenda kuwasihi Watanzania wote na wadau wa maendeleo kusoma kitabu hiki ili tupate kutumia mafundisho ya Sokoine katika kuboresha utendaji wetu wa kazi ili kuleta maendeleo ya Taifa letu na kuimarisha ustawi wa wananchi,"amesisitiza Waziri Simbachawene.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news