DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Baraka Ildephonce Leonard kuwa Katibu wa Bunge akichukua nafasi ya Nenelwa Mwihambi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Viongozi walioteuliwa Mwihambi na Baraka wataapishwa Septemba 19, 2024 saa 09.00 alasiri, Ikulu jijini Dar es Salaam.