Rais Dkt.Samia afanya uteuzi TTCL,NARCO,UCSAF,TEMDO, ATCL na Shirika la Posta

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 25, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Sharifa Nyanga, Mheshimiwa Rais amemteua David Chimbi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).

Pia, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Salim Milanzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Balozi Valentino Longino Mowola kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano (UCSAF).

Wengine ni Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO) na Prof. Neema Mori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kipindi cha pili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news