BEIJING-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika na China mkutano unaotarajiwa kuanza Septemba 4 hadi 6,2024.

Vilevile, Rais Samia atafanya mazungumzo na Rais China, Mhe. Xi Jinping na kushuhudia uwekaji saini wa Hati za Makubaliano ya Uboreshaji wa Reli ya TAZARA.
Katika hatua nyingine,Mheshimiwa Rais Dkt.Samia atakutana na makampuni na wawekezaji kutoka China ili kuhamasisha uwekezaji zaidi nchini Tanzania.