RC Chongolo awezesha ujenzi wa kanisa Makambako

NJOMBE-Fedha zaidi ya shilingi milioni 12.3 zimepatikana katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mashujaa lililopo Kata ya Kivavi mjini Makambako mkoani Njombe.
Katika harambee hiyo,mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Mheshimiwa Daniel Chongolo akichangia kiasi cha shilingi milioni nne.

Katika fedha hizo kiasi cha shilingi 5,790,000, fedha taslimu kimepatikana huku ahadi ikiwa ni shilingi milioni 6,540,000,

Akiwasilisha mchango huo Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo ambaye ni Diwani wa Kata ya Kivavi,Alimwimike Sawhi amesema, Chongolo amechangia kiasi hicho baada ya kualikwa kuwa mgeni rasmi, huku akitaka kanisa hilo kutumika kurejesha maadili mema katika jamii.

Mchungaji wa kanisa hilo,Raphael Migodela amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Songwe,Mheshimiwa Daniel Chongolo kwa mchango huo na kueleza kuwa kanisa hilo litakuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kuachana na imani za kishirikina ambazo zinepelekea mauaji kwenye jamii.

Nao baadhi ya waumini wa kanisa hilo,Godfrey Mabena, Flora Mwakanyamale wamewataka viongozi wa serikali na kisiasa kuwekeza kwenye ujenzi wa makanisa,kwani huko ndio chanzo cha amani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news