RC Kunenge azindua Kliniki ya Ardhi na kutatua migogoro Vikindu

PWANI-Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amezindua Kliniki ya Ardhi katika Kata ya Vikindu wilayani Mkuranga kwa lengo la kusaidia wananchi wa wilaya hiyo kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi inayowakabili.
Uzinduzi wa kliniki hiyo umefanyika mwishoni mwa wiki Kata ya Vikindu ambapo alipata wasaa wa baada ya uzinduzi wa kusikiliza malalamiko ya wananchi.

Sambamba na kutoa mwongozo wa utatuzi kwa kuwataka viongozi wa wilaya kufuatilia kwa umakini migogoro hiyo, ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria.

Kunenge pia aliwahimiza wananchi wa Kata ya Vikindu kujitokeza kwa wingi kutumia huduma za kliniki hiyo ili kurasimisha maeneo yao kwa kufuata taratibu za kisheria. "Jitokezeni kwa wingi ili mpate haki ya kukaa kwenye maeneo rasmi," alisema Kunenge.

Aidha, aliwahimiza wananchi kutumia fursa hiyo kutatua migogoro ya ardhi, kwani wapo wataalamu wa masuala ya ardhi ambao wako tayari kuwasaidia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bi Hadija alisema kuwa,baada ya uzinduzi huo, kambi ya wataalamu itakaa katika Kata ya Vikindu kwa siku nane, ili kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za ardhi zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.

Bi.Hadija pia alimuomba Mkuu wa Mkoa, Abubakar Kunenge, kuongeza idadi ya wataalamu wa ardhi, kwani waliopo kwa sasa hawakidhi mahitaji ya wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news