Rushwa ya shilingi milioni 1 yamponza Afisa Mtendaji mtaa wa Pugu Kinyamwezi

DAR- Bakari Heriel Mchome ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mtaa Pugu Kinyamwezi jijini Dar es Salaam ametiwa hatiani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni 1.
Ni kutoka kwa mwananchi ili aweze kumpatia orodha ya majina ya watu waliovamia eneo lake lililopo Pugu Kinyamwezi.

Hukumu yake imetolewa Agosti 30,2024 kupitia kesi ya Jinai namba 96/2023 ambayo ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Bittony Mwakisu.

Aidha,shauri hilo liliendeshwa na mawakili wa Serikali Waandamizi, Veronica Chimwanda na Fatuma Waziri ambapo mshtakiwa Bw. Bakari Heriel Mchome,Afisa Mtendaji wa Mtaa Pugu Kinyamwezi alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 15(1) (a) na (2) Cha PCCA [Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022].

Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya shilingi 500,000 au kwenda gerezani miaka mitatu.Mshtakiwa amelipa faini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news