Serikali imewasogezea fursa kupitia PPP, changamkieni-Kayombo

NA JOSEPHINE MAJURA
WF Simiyu

KATIBU- Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Prisca Kayombo, amewataka Watanzania kuchangamkia fursa zilizoainishwa katika Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi (PPP) ili kuweza kujikwamua kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyohusisha Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,Sura NA. 103 na Matumizi sahihi ya Takwimu ulioandaliwa na Wizara ya Fedha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Simiyu).

Bi. Kayombo alitoa rai hiyo mkoani Simiyu, wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyojumuisha Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.

“Serikali iliona mapungufu katika Sheria ya Ubia kati ya Serikali na Sekta ya Binafsi ndiyo maana imefanya marekebisho ambayo yanatoa fursa kwa Watanzania kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini,”alisema Bi. Kayombo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Prisca Kayombo, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi,Sura NA. 103 na Matumizi sahihi ya Takwimu iliyohusisha Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.

Alisema kuwa,marekebisho ya Sheria hiyo yanatoa fursa kwa Watanzania kufanya uwekezaji nchini ili kusaidia uchumi wa Tanzania kuimarika na kuipunguzia Serikali matumizi ya fedha za kigeni kwa kuwalipa Wawekezaji wa nje ya nchi.

Akizungumzia suala la matumizi sahihi ya Takwimu, alisema kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikiitumia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuandaa takwimu rasmi ambazo hutumiwa na Serikali kurahisisha kupanga bajeti na mipango ya kimaendeleo kwa wananchi wake.
Afisa Sheria Mkuu, Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha Bw. Paul Kimweri, akimshukuru Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Prisca Kayombo (katikati) ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyohusisha Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Bw. Alred Misana, ulioandaliwa na Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano m, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.

Kwa upande wake Afisa Sheria Mkuu, Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bw. Paul Kimweri alisema kuwa Serikali inaendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji mbalimbali wa Serikali katika mikoa yote nchini.

Aliongeza kuwa, kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, ulitanguliwa na Mkutano wa ufunguzi uliofanywa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambao uliwahusisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na viongozi wengine wa Serikali mkoani Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Bw. Alred Misana, akitoa mada kuhusu Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango, iliyohusisha Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara, mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kufanyika katika ukumbi wa Mikutano, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Simiyu.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Mipango na Uratibu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga m, Bw. Alex Mpasa, aliahidi kwenda kuzisimamia Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatekeleza Sheria hizo kama Sheria ilivyoelekeza.

Aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Mipango kwa kuwa mafunzo hayo waliyoyapata yatawasaidia kuwa na uelewa mpana wakati wa kutekeleza majukumu yao na kuwasaidia wengine ambao hawajapata mafunzo hayo.
Afisa Ugavi, Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bw. Raphael Chima, akifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Wakuu wa Idara ya Mipango iliyohusisha Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.

Wizara ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara ya Ununuzi na Mipango nchi nzima katika mikoa ya Kikanda ikiwemo Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Pwani, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Magharibi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news