Serikali inatekeleza ilani kwa vitendo-Waziri Lukuvi

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Williamu Lukuvi amesema ujenzi na uimarishaji wa wa miundo mbinu ya Maji Kata ya Mbezi ni kielelezo tosha kinachoonesha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza ilani ya chama kwa vitendo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Williamu Lukuvi akikagua Mradi wa Maji Mshikamano katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo wilaya ya Ubungo.

Waziri ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea Miradi ya Maendeleo ambapo ametembelea na kujionea Mradi wa Maji Mshikamano ulipo Kata ya Mbezi Katika Wilaya ya Ubungo jijini Dar e salaam na baadae kufanya Mkutano wa hadhara Mburahati tarehe 18/09/2023.

Shida ya maji Kata ya Mbezi ilikuwa tatizo kubwa hivyo kukamilika kwa Mradi wa Maji niliotembelea kwa 100% utahudumia watu zaidi ya laki mbili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Williamu Lukuvi akikagua Mradi wa Maji Mshikamano katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo wilaya ya Ubungo.
“Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan ametegua kitendawili hicho kwa Wananchi wa Ubungo kupata Maji safi na salama ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake hivyo niwape shime Wananchi muendelee kutangaza kazi njema zinazofanywa na Serikali,” alisema Waziri Lukuvi.

Kazi hizi zinazofanywa na Serikali zinapaswa kuonekana na kutangazwa ili Watanzania wengine waone kazi mbalimbali kwa mifano na Falsafa ya Mhe. Rais ya Kazi iendelee inaendelea kutekelezwa kwenye miradi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Williamu Lukuvi akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika Mburahati jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) Ubungo amesema kupitia mradi wa Metroplitan Development Project (DMDP) Awamu ya Pili utajenga kingo za Mto Gide na Mto China huko Makurumula,

Aidha kwa kupitia Mradi wa (DMDP) kwa upande wa Ubungo kuna barabara 21 zitakazojengwa ikiwemo barabara nne kubwa katika Kata ya Kimara ambazo ni barabara ya lami Suka, Barabara ya Mlingo, barabara ya Milenia ya tatu, alisema Waziri Kitila.

Naye Mhe. Issa Mtemvu (Mb) Kibamba amesema, Wilaya ya Ubungo ilikuwa na wastani mdogo wa upatikanaji wa maji, lakini Mhe. Rais amechukua kilio cha wakazi wa Ubungo na leo miradi imekamilika.

“Serikali haikuwaacha Wananchi wa Goba na viunga vya Salasala katika ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye ujazo wa lita zaidi ya milllioni sita eneoTegeta A hivyo tunamshukuru sana Mhe. Rais, Dkt Samia,” amesema Mtemvu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Williamu Lukuvi akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe Hassan Bomboko wakati wa Mkutano wa Hadhara Mburahati jijini Dar es Salaam.

"Wabunge tumepata bahati tunaomba fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo Serikalini na tunazipata, ahadi yetu ni kuendelea kumunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan."

Awali Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe Hassan Bomboko amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa na zuri kwa kuleta miradi ya maendeleo ambayo imechagiza mabadiliko makubwa kwa sekta mbalimbali.

Wananchi wa wilaya ya Ubungo wana deni kwa Mhe, Rais kutokana na kazi kubwa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyofanya na Serikali ya Awamu ya Sita, kwa dhamira ya kweli na ya dhati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Williamu Lukuvi akikagua Mradi wa Maji Mshikamano katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo wilaya ya Ubungo.

“Hakuna kata ambayo haijaguswa kabisa kwa upande wa mradi iwe ni upande wa Elimu, Maji, Barabara Afya au Miradi mengine ya Maendeleo,” amesema Mkuu wa wilaya, Bomboko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news