Serikali yaahidi kuendelea kuipa kipaumbele Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)

ARUSHA-Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kuahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuipa kipaumbele kwa kuwa huduma za hali ya hewa zinasaidia katika mipango mbalimbali ya maendeleo.
“Wataalam wa hali ya hewa mnafanya kazi nzuri, utabiri unaotolewa hivi sasa ni wa usahihi na umesaidia sana katika masuala ya kiuchumi na kijamii na mipango ya nchi kwa ujumla.”

Dkt.Nchemba ameyasema hayo Septemba 12,2024 alipotembelea banda la TMA katika viwanja vya AICC, Arusha wakati akifunga rasmi Jukwaa la 16 la Ununuzi la Afrika Mashariki.
"Matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa ni suala mtambuka,kwani husaidia katika mipango na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamiii hususani katika kupunguza madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa kwa umma."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news