Serikali yakamata madini ya dhahabu kilo 15.78 bandari yakitoroshwa

DAR-Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde ametangaza kukamatwa kwa madini ya dhahabu kilo 15.78 bandarini yalipokuwa yakitoroshwa.Waziri Mavunde amesema hayo leo tarehe 11 Septemba, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari.

"Nchi yetu inazo sekta kadhaa za uzalishaji ambazo mapato yake ndiyo msingi wa maendeleo ya uchumi wetu ikiwemo sekta ya madini. Sasa basi, tunapokuwa na watu wachache ambao wanajihusisha na vitendo vya utoroshaji wa madini kuikosesha Serikali mapato hatuwezi kuwavumilia," amesema Mavunde.
"Kilo hizo 15.78 kwa bei ya leo zina thamani ya takribani bilioni 3.4 fedha ambazo kwa sasa zote watoroshaji hawa wanakwenda kuzipoteza.

"Serikali tunakwenda kufuta leseni zao wakitiwa hatiani na mahakama na kuwaweka kwenye orodha ambayo hawataruhusiwa kumiliki Leseni ya kufanya biashara yeyote katika mnyororo wa thamani wa madini Nchini Tanzania,"amebainisha Mavunde.
Akielezea kuhusu uchunguzi unaoendelea, Waziri Mavunde ameeleza kuwa, watuhumiwa wamesema madini hayo ya dhahabu walikuwa wanasafirisha kutoka bandari ya Dar es Salaam kuelekea Visiwani vya Zanzibar.

Mavunde amefafanua kuwa, kwa sasa uchunguzi na Mahojiano kwa watuhumiwa unaendelea na pindi kazi hii ikikamilika tutawapandisha mahakamani ili kujibu mashtaka husika.
Sambamba na hapo, Waziri Mavunde amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Kikosi kazi cha kuzuia utoroshaji wa madini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama

Waziri Mavunde ametoa rai kwa wafanyabiashara nchini kuacha tabia ya utoroshaji madini kwasababu inarudisha nyuma juhudi za Serikali za kukuza uchumi wa nchi yetu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news