Serikali yasisitiza umuhimu wa takwimu rasmi katika mipango na shughuli za kiuchumi

NA ASIA SINGANO
WF-Morogoro

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, amewataka Watanzania kutumia Takwimu rasmi katika mipango na shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kupunguza athari zinazotokana na kufanya mipango ya maendeleo bila kuzingatia takwimu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, akifungua Mkutano wa Kanda ya Pwani, uliyofanyika katika mkoa wa Morogoro, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Fedha, ambapo umehusisha Wakuu wa vitengo vya Usimamizi na Ugavi, Wakuu wa Idara za Mipango, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri, baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha, watumishi kutoka Ofisi ya Takwimu Tanzania, wawakilishi kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi pamoja na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Dkt. Mussa aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Kikanda, Kanda ya Pwani, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu rasmi zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu Kanda ya Pwani, uliyofanyika mkoani Morogoro.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Pwani Bi. Vicky Mollel, akiteta jambo na Afisa Ugavi Mkuu, kutoka Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi. Fatuma Msantu, wakati wa mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ambapo katika Kanda ya Pwani, mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Aliitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kutoa kipaumbele kwa makundi maalumu ikiwemo vijana, wanawake, watu wenye ulemavu katika masuala ya Ununuzi wa Umma ili kuwainua na kuendelea kukuza uchumi.

"Ni vyema watu wa ununuzi waendelee kutoa fursa kwa makundi maalumu katika masuala ya ununuzi ikiwemo kuwaelimisha kuhusu fursa ziizopo katika ununuzi wa umma,’’alisema Dkt.Mussa.
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Pwani Bi. Vicky Mollel, akitoa ufafanuzi kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, kwa washiriki wa Mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, wakati wa Mkutano wa Kikanda, Kanda ya Pwani uliyofanyika mkoani Morogoro.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Pwani, Bi. Vicky Mollel, alisema katika sheria ya ununuzi wa umma namba 10 ya mwaka 2023, Serikali imeweka fursa nyingi kwa ajili ya watu na kampuni za ndani ikiwemo kutenga zabuni takribani bilioni 50 ili kuongeza kipato kwa wananchi na kukuza uchumi wa nchi.
Mtakwimu Mkuu, kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Moris Mulilo, akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa Takwimu kwa washiriki wa mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa mkutano huo Kanda ya Pwani uliyofanyika mkoani Morogoro.

"Fursa hizo ni pamoja na kutenga zabuni za mpaka bilioni 50 kwa ajili ya Watanzania, kwa kazi za ujenzi, ununuzi wa bidhaa pamoja na huduma mbalimbali, kampuni zetu za ndani zimepewa fursa ya kuungana na kampuni za Nje au kuingia ushirika na kampuni za Nje ili kujenga uwezo wa kufanya kazi na zitakuwa kampuni kiongozi,’’alisema Bi. Vicky.
Washiriki wa Mkutano wa Kikanda, Kanda ya Pwani, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, wakifuatilia mkutano huo mkoani Morogoro.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maandalizi ya Uchambuzi wa Miradi Kituo cha Ubia (PPPC), Bw. Augustino Saibull, akizungumza wakati wa mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Naye Afisa Ugavi Mkuu, kutoka Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi. Fatuma Msantu, amewataka Wakuu wa Mipango pamoja na Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi kufuata sheria za ununuzi wa Umma na kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NeST).

"Na waachane na zile tabia za kutokutumia (NeST), ni muhimu, lazima waitumie ambapo pia itaweza kuwachukua hata wale wazalishaji wadogo ambao nao tunawahimiza waingie kwenye NeST ili waweze kuonekana wakati wazabuni wanapokwenda kwenye hizo zabuni zao,"alisema Bi. Msantu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa (wapili kulia waliyoketi), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, wakwanza kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Pwani Bi. Vicky Mollel, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya maandalizi na Uchambuzi wa Miradi, Kituo cha Ubia (PPP Center) Bw. Augustino Saibull (wakwanza kushoto), Afisa Ugavi Mkuu, Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha Bi. Fatuma Msantu (wapili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya maandalizi na Uchambuzi wa Miradi, Kituo cha Ubia (PPP Center) pamoja na washiriki wengine, baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Picha na matukio mbalimbali katika Mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura No. 410, Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura No 103 na matumizi ya Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kanda ya Pwani, uliyofanyika mkoani Morogoro ambapo mkutano huo unafanyika katika kanda zote hapa nchini ambapo kila kanda mkutano huo utafanyika katika mkoa mmoja na kujumuisha washiriki wa mikoa ya Kanda husika.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha - Morogoro).

Kabla ya Mikutano ya Kikanda inayoendelea kufanyika, ulianza mkutano kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi sahihi ya Takwimu rasmi kwa Wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa, na Waganga Wakuu wa Wilaya jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck nchemba (Mb).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news