Shilingi milioni 780 kuboresha huduma ya maji Marangu Mashariki

KILIMANJARO-Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) imekusudia kutekeleza mradi wa majisafi wenye lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi kwenye vijiji vya Samanga, Rauya pamoja na Ashira vilivyoko kwenye Kata ya Marangu Mashariki Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
Mradi huo unategemewa kuzalisha mita za ujazo lita 4,320 kwa siku na utahudumia zaidi ya wananchi 10,574.

Mradi huo utakaotekelezwa kwa awamu mbili zikihusisha kuboresha vyanzo viwili vya maji vya Kerya pamoja na Lyasongoro, ulazaji wa bomba kuu la usambazaji majisafi umbali wa kilomita l7.35 kutoka kwenye vyanzo hadi eneo la tanki la maji la Samanga Makao Makuu.

Mradi huo unategemea kukamilika Oktoba, 2024 kwa awamu ya kwanza na utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo itaanza Novemba, 2024 na kukamilika Januari 2025 itakayohusisha uchimbaji.

Sambamba na ulazaji wa bomba yenye vipenyo mbalimbali ili kuwasogezea wananchi huduma pamoja na ujenzi wa vituo vipya vya kupunguza kasi ya maji yaani BPT.

Mamlaka imeshirikiana na wananchi na viongozi wa kata hiyo kama wanavyobainisha kwenye ziara ya Kamati ya Maendeleo ya Kata ilipotembelea na kujionea utekelezaji wa kazi mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news