Shirika la SOS Children’s latembelea Bugando

MWANZA-Shirika la SOS Children’s Village la jijini Mwanza wakiongozwa na Meneja Miradi wao Bw. John Masenza, wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando katika idara ya watoto chumba cha uangalizi maalumu (NICU) na kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo nguo za watoto, pampasi, taulo za kike pamoja na mafuta ya kujipaka.
Zoezi hilo limefanyika mapema Septemba 12,2024 lengo likiwa ni kudumisha mashirikiano ya muda mrefu baina ya SOS Children’s Village na Hospitali ya Bugando.

Aidha, Bw. Gaspar Mshana ambaye ni Afisa Ustawi Hospitali ya Bugando ameshukuru uongozi wa Shirika la SOS kwa msaada na kujali watoto hao na kusema kuwa,misaada hii inasadia kupunguza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wazazi wa watoto hao hasa wanapokuwa hospitalini pamoja na kusaidia kudumisha maisha yao kuwa bora.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news