Simba SC na Al Hilal zatoshana nguvu

DAR-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imetoshana nguvu na Al Hilal kutoka nchini Sudan kwa kutoka sare ya bao 1-1.
Ni kupitia mtanange wa kirafiki wa Kimataifa uliopigwa Agosti 31,2024 katika Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.

Simba SC walianza mchezo kwa kasi huku wakiliandama lango la Al Hilal ingawa walikuwa imara kuzuia mashambulizi.

Leonel Ateba alitupia bao la kwanza dakika ya 26 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi.

Aidha,kipindi cha pili walianza kwa kasi huku Al Hilal wakifanya mashambulizi kadhaa langoni mwao.

Suliman Ezzala hakuweza kuendelea na mchezo baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 53, baada ya kumchezea madhambi Augustine Okajepha.

Sergie Pokou aliisawazishia Al Hilal bao hilo dakika ya 75 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kumzidi ujanja mlinzi Kelvin Kijili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news