Simba SC yaichapa Dodoma Jiji FC bao 1-0

NA DIRAMAKINI

BAO pekee la Jean Charles Ahoua limeiwezesha Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam kujizolea alama tatu kwa Dodoma Jiji FC.
Ahoua alitupatia bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 62 baada ya nahodha Mohamed Hussein kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Mtanange huo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji umepigwa Septemba 29,2024 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Ikumbukwe,mchezo huo ulianza kwa kasi huku Simba SC ikifanya mashambulizi langoni mwa Dodoma,lakini walikosa umakini wa kutumia nafasi walizopata.

Aidha,baada ya bao hilo,Simba SC waliendelea kuliandama lango la Dodoma na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa wenyeji hao.

Katika mechi hiyo kiungo mshambuliaji Deborah Fernandez amechaguliwa nyota bora wa mchezo.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema, mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ulikuwa mgumu, lakini amewapongeza wachezaji kwa kujituma muda wote.

Kocha Fadlu amesema,walikuwa na uwezo wa kupata ushindi mnono wa zaidi ya mabao manne mpaka matano,lakini hawkuweza kuzitumia vizuri nafasi walizopata ugenini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news