TRIPOLI-Mechi ya kwanza ya Simba SC katika Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli Sports Club imemalizika kwa sare ya bila kufungana.
Mtanange huo umepigwa Septemba 15,2024 katika Uwanja wa Kimataifa wa Tripoli nchini Libya.
Mchezo ulianza kwa kasi huku wenyeji Al Ahli Tripoli wakishambulia kwa kasi,lakini safu ya ya ulinzi ya Simba SC ilionekana kuwa imara zaidi.
Kuanzia dakika ya 20, Simba SC ilitawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Al Ahli Tripoli ingawa hawakuweza kuwa makini kwenye kutoa pasi za mwisho.
Aidha,kipindi cha pili wenyeji Tripoli walirudi kwa kasi na kuongeza presha kwenye lango la Simba SC,lakini walionekana kuwa makini kuhakikisha wanalinda na kutoruhusu bao.
Baada ya mchezo huo kumalizika,Simba SC wanarejea nyumbani kujipanga na mechi ya marudiano itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 22,2024.